Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg awashukuru Lamar, Drake

IMG 0851.jpeg Snoop Dogg awashukuru Lamar, Drake

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki na producer kutoka Marekani Snoop Dogg amewashukuru wasanii wenzake Kendrick Lamar na Drake kwa kurudisha muziki kwenye mstari.

Akiwa kwenye mahojiano yake na ‘Entertainment Tonight’, Snoop ameeleza kuwa kufuatia na bifu la wawili hao limepelekea kurudisha tasnia ya muziki katika mstari wake huku akikazia kuwa nyimbo ambazo walizokuwa wakizitoa za kurushiana madongo ziliimarishwa kuanzia uandishi hadi uandaaji.

Hata hivyo aliwashukuru Drake na Kendrick Lamar kwa kurudisha muziki wa Hip-hop katika chati na kuufanya usikilizwe zaidi duniani kote.

Ikumbukwe kuwa bifu la wawili hao lilianza baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomsapoti Drake kupitia album yake ya ‘For All The Dog’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live