Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg atangaza kutoa albamu ya injili

1916 Snoop Dogg Gospel Album2

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mwaka jana, Snoop Dogg alitangaza kwamba anataka kuingia kwenye ulimwengu wa Injili na ataoa albamu kuhusiana na mada hiyo.



Snoop jana katika kipindi cha Beats 1 alisema kwamba anaifanyia kazi albamu yake ya injili kwa ajii ni kitu ambacho moyo wake umekuwa ukitaka kufanya kwa muda sasa. Snoop aliongezea kwa kusema kuwa hakuwahi kupata muda wa kufanya kazi hiyo kwa sababu hapo awali amekuwa akifanya biashara ya kigangsta na aliongezea kwa kusema kuwa kuimba injili ni kitu ambacho kilikuwa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na ameamua kufanya hivyo sasa.



Snoop amesema kuwa albamu hiyo anaifanyia kazi kweli na itaitwa Bible of Love. Kama Snoop ataweza kukamilisha albamu hiyo basi atakuwa amerekodi jumla ya albamu kumi na sita ndani ya studio. Mashabiki watapata ladha kwa mara ya kwanza ya albamu hiyo siku ya maadhimisho ya 19 ya Super Bowl mwezi Februari. Tukio hilo litafanyika kwenyw ukumbi mubwa uitwao Benson Great Hall uliopo Chuo Kikuu cha Betheli huko St. Paul, Minnesota siku ya Februari 1 mwaka huu.



Snopp ataungana na baadhi ya wasanii wa injili akiwemo Tye Tribbett, Sisters Clark, Faith Evans na Rance Allen katika siku ya kuzindua albamu yake.na uzinduzi huo utarushwa katika chaneli ya BET tarehe 3 Februari mwaka huu.



Na Raheem Rajuu

Chanzo: bongo5.com