Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg alipoteza fahamu baada ya kumuona 2 Pack

Snoop Dogg NA 2PAC Snoop Dogg na 2 Pack

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Snoop Dogg amefunguka kwamba alipoteza fahamu baada ya kumuona Tupac Shakur akiwa mahututi hospitali mara baada ya kupigwa risasi September 7, 1996.

Akizungumza kwenye podcast ya Logan Paul ‘Impaulsive’ Snoop Dogg amesema kabla ya kufika alihisi mambo yataenda kuwa sawa lakini baada ya kumuona mshkaji wake anapumulia mpira ndipo alihisi hali sio shwari.

Mama mzazi wa Tupac Shakur alimchukua na kumpeleka bafuni kwa ajili ya kuzungumza naye namna ya kuwa imara juu ya jambo lile.

Baadaye Snoop alirejea kwenye nguvu na kwenda kuzungumza na Tupac ambaye walikuwa marafiki wakubwa. Na hiyo ilikuwa ndio mara ya mwisho kuzungumza naye, September 13 alitangazwa kufariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live