Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skales: Nimetembea na Wanawake zaidi ya 100

Skales Pic Kutoka nchini Nigeria, mwanamuziki Skales

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka nchini Nigeria, mwanamuziki Skales, amewashtua baadhi ya mashabiki zake baada ya kuweka wazi kuwa ameshakuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya wanawake 100.

Staa huyo wa ngoma ya ‘Shake Body’ alifichua hayo kwenye mahojiano na kipindi cha 'Drip Check'.

"Nahisi kama nimekuwa baba maisha yangu yote. Nimekuwa nikiwatunza wanawake maisha yangu yote {akacheka}, kwasababu nimekuwa kwenye uhusiano na wanawake zaidi ya 100."

“Nilifanya mambo mengi ya kitoto. Unatarajia nini kutoka kwa kijana ambaye ni maarufu na anaweza kupata kila kitu ikiwa ni pamoja na wanawake?”

“Kuna wanawake wengi wazuri ambao nimewapoteza kwa sababu ya tabia yangu ya kitoto. Lakini kwa sababu ya uzoefu huo, nimekuwa mwanamume bora.” amesema Skales.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live