Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siwezi kwenda WCB, Kings - Chid Benz

6ef38687f577fc85885a26c2a0ddae6f Siwezi kwenda WCB, Kings - Chid Benz

Thu, 3 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa Bongo fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’amesema kulingana na muziki anaoimba hawezi kukubali kujiunga na lebo kubwa nchini.

Chid Benz alizitaja lebo hizo ni WCB inayomilikiwa na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Kings Music ya Ali Kiba na Konde Gang ya Rajab Kahali, Harmonize ambazo amesema hawezi kujiunga nazo.

“Nina uwezo mkubwa wa kuimba kila mmoja anajua hata nikipata bahati ya lebo moja ikataka nijiunge siwezi kukubali kufanya hivyo, kwanza najitegemea lakini pia nafanya muziki wa tofauti na wao,” alisema.

Alisema kwa sasa anaendelea kujipanga kuhakikisha anatoa kazi ambayo ana amini itamrudisha kwenye mstari kama alivyokuwa miaka ya nyuma.

Alisema kipindi cha nyuma kuna baadhi ya watu walikuwa wanamuongelea mambo mabaya kwenye mitandao lakini hawezi kuwafuatilia kwa sababu hawamtakii mema kwenye tasnia hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz