Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siwezi kumwacha mume wangu kisa mchepuko - mke wa DJ Allly B

Rty Ally Bbbb Siwezi kumwacha mume wangu kisa mchepuko - mke wa DJ Allly B

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama Simba ambaye ni Mke wa Dj maarufu Bongo Dj AllyB, amefunguka namna ambavyo hatishiki na michepuko inayomnyemelea mume wake baada ya kupata pesa na kuwa maarufu.

Mama Simba amesema anafahamu kama mumewe lazima atakuwa na michepuko yake katika sehemu mbalimbali anazofanyia kazi na hilo halikwepeki kutokana na ukubwa wa jina lake kwasasa mjini. Lakini hiyo haimshitui wala kumnyima usingizini kikubwa anapewa heshima kama mke halali na anafanyiwa vitu vyote anavyotakiwa kufanyiwa mwanamke.

Kipi bora? Kuondoka kwenye ndoa kisa mumeo kakuchiti alafu kwenda kuwa kwenye mahusiano na mume wa mtu au kuchitiwa na mume wako alafu unaheshimika kiasi kwamba hata michepuko inakuogopa"- amehoji.

Kisha akaongeza kwamba yeye na mume wake wametoka mbali, ni miaka saba sasa tangu wakutane na kuanzisha maisha, amemzalia watoto wawili, anamjua tangu akiwa masikini hadi alipopata pesa, amehusika pakubwa kumuombea afanikiwe hadi leo hii wanamiliki nyumba na magari alafu amuache kirahisi kisa kuchitiwa? Bi Simba amesema hilo halitakuja kutokea.

Amewataka vimada wa mjini wanaotembea na mume wake kama wapo, basi wachiti tu kikubwa wawe na heshima na mipaka juu ya ndoa yake, wala hamuonei wivu akiondoka kwasababu akiendekeza kumpekua atajikuta anashindwa maisha ya ndoa.

Yote tisa, kumi ni kwamba siyo kwamba hampendi mumewe, anampenda sana ndiyo maana anafanya hivyo ili ndoa yake idumu milele kwasababu ukiuchunguza sana mnofu huwezi kuula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live