Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sitamgeza mtu yeyote-Vanillah

Vanillah Sitamgeza mtu yeyote-Vanillah

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mpya ambaye ametambulishwa Kings Music, Fanuel Peter ‘Vanillah’ amesema ameingia kwenye muziki kuleta ladha yake ya muziki mzuri.

Hayo ameyasema alipofanya mahojiano na televisheni za mitandaoni ambapo amesema, kwa kipindi cha takriban mwaka mzima aliokaa kabla ya kutambulishwa amepikwa akapikika.

“Nimejifunza mambo mengi na hasa nilianzia kwenye albamu ya Alikiba ya Only One King baada ya prodyuza Yogo kuniambia niingize kitu kwenye hiyo albamu na kweli kikakubalika na mpaka sasa niko hapa,” alisema Vanillah.

Akielezea historia yake kwa kifupi, Vanillah alisema amezaliwa Mwanza na kukulia Mwanza. Asilimia nyingi za maisha yangu amekulia Mwanza.

“Nilikutana na Ally ilikuwa Dar, nilikuwa nafanya kazi na Yogo. Only One King. Yogo akaniambimbia nishiriki kwenye albamu hiyo, nikaonesha na bahati nzurui wakaona ninafaa,” alisema Vanillah ambaye ameachia EP yake inayokwenda kwa jina la Nisikilize Mimi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live