Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sitaki tena tuzo Tanzania – Mr. Blue

1911 20766661 371887279895071 2219534997155479552 N TZW

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Mr. Blue amesema kwa sasa hataki tena kupatiwa tuzo kutoka Bongo kutokana na kunyimwa kwa muda mrefu.



Mr. Blue ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa amekuwa kwenye game kwa muda mrefu na hakupatiwa tuzo na alipofika kwa sasa kimuziki haoni kama kuna tuzo anaweza kupatiwa.

“Sitaki tena tuzo, yaani is too long nimesubiri kwa muda mrefu, Tanzania I don’t need any tuzo, kuna tuzo gani ya kunipa mimi, utanipa tuzo ya wimbo bora wa mwaka huu ‘Mbwa Koko’ hizo nyingine za nyuma unazifanyia nini?,” amesema.

“Kwenye game nimeanza toka nimekuwa mtoto mpaka nimekuwa na watoto bado nasubiri, siwezi tena kuwa na hamu ya kuitaka tuzo sasa hivi ninachoangalia ni mambo mengine, niwepo tu hata sifanyi tena kwa ajili yangu,” ameongeza.

Mr. Blue kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Mbwa Mkoko.

Chanzo: bongo5.com