Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Sitaki tena muziki, ni haramu" - Kali P

ABD "Sitaki tena muziki, ni haramu" - Kali P

Wed, 28 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Msanii aliyetamba na ngoma ya imekaa vibaya na tumbo joto Abdul Miraji maarufu kama Kali P amesema hataki tena kusikia masuala ya muziki kwani katika upande wa dini yake ya kiislam ni jambo hilo ni haramu.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatano , 28th Apr , 2021 Picha ya aliyekuwa msanii Kali P

Akizungumza na BigChawa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Kali P amesema ameamua kumrudia Mungu na sasa hivi ana takriban miaka 12 ameingia dini na ameachana na masuala ya muziki.

"Katika dini yetu ya Uislam muziki ni haram ndio maana mimi nikajitoa kwa sababu ya kumuogopa Mungu, kama ujumbe kuna njia ya watu kuwafikishia ila sio muziki, siku ambayo naacha muziki nafsi yangu ilisema sipendi tena muziki"

Aidha msanii Kali P ameongeza kusema "Kipindi nafanya muziki nilikuwa na miaka 22, Nyimbo zangu zikipigwa najisikia vibaya na sina habari nazo tena, atakayeimba atakuwa anajichochea moto mwenyewe, muziki sio utaratibu halali wa kutafuta riziki, baraka kubwa ni kumtambua Mungu".

Kwa sasa aliyekuwa msanii huyo anafahamika kwa jina la Shekh Abdul Miraji na anapatikana maeneo ya Kitunda, Dar es Salaam.

Chanzo: eatv.tv