Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Siogopi manyaku nyaku,nitaolewa" - Hamisa Mobetto

11814 Mobeto+pic "Siogopi manyaku nyaku,nitaolewa" - Hamisa Mobetto

Mon, 1 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na mrembo Hamisa Mobetto ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa kwenye maisha yake anaogopa vitu vingi ila haogopi suala la mwanamke "manyaku nyaku" kumchukulia mwanaume wake.

Hamisa Mobetto amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hataweza kumuonyesha pia tayari kuolewa kama atakuwa amepangiwa hivyo. "Nipo kwenye mahusiano sidhani kama naweza nikaogopa manyaku nyaku, katika vitu ambavyo naweza nikaviogopa vipo vingi lakini sio mwanamke kunichukulia mwanaume wangu, kama akiamua kuondoka ni mipango ya Mungu na hakupangwa kuwa wangu lakini sio niogope mwanamke mwingine kwamba atakuwa naye" amesema Hamisa Mobetto

"Mpaka sasa hivi sijaolewa, kila kitu kinatokea kwa sababu yake na mipango ya mungu kwa jinsi tunavyoishi zaidi ndiyo unajifunza na kukua na sijajua mipango yangu ya ndoa ipoje ila mwanamke kuoelewa ni lazima na nitaolewa na mwanaume ambaye nimepangiwa"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live