Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Sio tu damu, hata figo nakutolea" Harmonize amhakikisha Poshy Queen

Harmonizeeee (1) "Sio tu damu, hata figo nakutolea" Harmonize amhakikisha Poshy Queen

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize na mpenzi wake mpya Poshy Queen wanaendelea kubalizi kwenye ufukwe wa mahaba kwa kutumiana jumbe tamu katika mitandao ya kijamii.

Baada ya Harmonize kufichua maelezo ya kina kuhusu huba lao, Poshy naye amejimaliza kwa kuichapisha picha ya Harmonize kwenye Instagram yake na kumtaja kuwa mwanamume wake wa kwanza kabisa Adamu.

“Adamu wangu mimi hapa,” Poshy Queen aliandika baada ya kuchapisha picha ya bosi huyo wa Konde Gang.

Harmonize naye hakuachwa nyuma, alitanua mbavu zake akisema kwamba yuko tayari leo kesho kumtolea mrembo huyo si tu damu bali hata figo mradi tu aendelee kumuona akimtabasamia.

Harmonize alifichua kwamba safari yao ya mapenzi ilifaa kuanza mwaka 2017 lakini kwa njia moja au nyingine ikakwamizwa, bila wao kujua kwamba walikuwa wanatayarishwa kupendana vizuri mwaka 2024.

Msanii huyo alisema kwamba ambacho amejifunza kutoka kwa penzi hilo jipya ni ustahimilifu, akisema bintiye, Zuuh Konde atafurahi kumpata mama wa kambo mpya.

“Sio tu damu, hata figo nakutolea Eva wangu. 2017 na sasa tuko hapa. Ni historia iliyoje kuwaambia wanetu Nova na Zuuh Konde, ni sharti wawe wastahimilifu. Mapenzi ni ukichaa,” Diamond alimjibu.

Baadhi ya watu kwenye ukurasa huo bado wangali na maruweruwe ya kuamini kama wawili hao wako kwenye mapenzi kweli ama ni biashara tu wanafanya kwa matayarisho ya video ya wimbo mpya wa Marioo aliomshirikisha Harmonize.

Wengine walisema Harmonize hajafuata mapenzi pale bali ni maumbile tu, kwani kwa muda mrefu amekuwa akionekana kuwapenda wanawake si tu kwa sababu ya mapenzi bali kwa sababu ya muonekano wao mzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live