Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio Mapiano tu, Fid Q ameimba mpaka Taarab

Fid Q Wasanii Data Fid Q

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku za Hivi Karibuni Jabali la #Rap nchini @therealfidq amezua mjadala mkubwa miongoni mwa Wadau wa muziki baada ya @chino_kidd7 kuomba wafanye goma Moja la #Amapino.

Wadau wengi wanaopinga na hata wanaokubaliana na #FidQ kupita kwenye dundo la Amapiano wamekuwa wakitoa mfano kuwa Fid Q amewahi kufanya #Taarab hivyo sio vibaya Akifanya Amapiano, Huku wale wanaopinga wakisema Fid Amewahi Kufanya Taarab lakini Amapiano hapana asifanye, Neno Taarab Linatajwa Sana.

Wimbo ambao unasemwa ni Taarab ni #Bambam ambayo amefanya na @ishamashauzioriginal , @richmavoko na @bigjahman1 na Producer ni Legend @marcochali_ Kutoka #MJRecords (@mjrecordstz ) lakini kiuhalisia wimbo ule sio Taarabu Bali ni #REGGAETON.

Baadhi ya Wadau wamekuwa wakisema kuwa wimbo ule ni Taarab (Labda Sababu Yupo #IshaMashauzi) lakini ukisikiliza Mdundo (Instrumental) ile Utagundua kuwa SIO TAARAB na Wala SIO FUSION Sababu hakuna Vionjo vyovyote vya TAARAB bali ni REGGAETON kabisa.

Aina ya Muziki huletwa na Instrumental na sio muimbaji hivyo uwepo wa Isha Mashauzi haufanyi wimbo wa #BamBam kuwa TAARAB.

Nadhani tuli/tuna-paswa (Kumpongeza) @ishamashauzioriginal ambaye yeye ndio Amepinduka na KUIMBA kwenye Dundo la Reggaeton vizuri Kabisa Huku yeye ni msanii wa Taarab na Amefit sana kama tunavyojua goma hili lili-hit Kila Jiji, Mkoa mpaka Chocho za mitaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live