Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sina tatizo na Nandy - Zuchu

ZUCHU NA NANDY Sina tatizo na Nandy - Zuchu

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

First lady wa Wasafi Classic Baby, Zuhura Othuman Soud ‘Zuchu’ amesema hana tatizo na msanii mwenzake wa kike Faustina Charles ‘Nandy’ kama ambavyo maneno yameibuka mitandaoni.

Alisema, akiwa nchini Ufarasa hivi karibuni aliona maneno kuwa Nandy alimtuma Mwijaku amponde yeye lakini haikumshtua kwani alijua ni masuala ya kimuziki tu.

“Niliona ni mambo tu ya kujitafutia ugali hivyo sikujali sana. Sina tatizo na Nandy na ninampongeza kwa kufunga ndoa,” alisema Zuchu.

Zuchu alisema hata kwenye harusi ya Nandy alishindwa kwenda kwa kuwa alikuwa na kazi lakini alialikwa.

“Nampongeza kwa kweli maana kuwa mjamzito halafu ni msanii na unaolewa sio kitu rahisi. Nimemwambia hata na mimi anipe hiyo duwa aliyoomba na mimi niombe,” alisema Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live