Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sina tatizo na Alikiba utimu wao haunihusu – Nay wa Mitego

3679 27581227 321140938378392 488490158404927488 N TZW

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amesema hana beef na Alikiba na wala hana timu yoyote katika muziki.



Nay ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mikono Juu’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yeye na Alikiba hawana tatizo lolote na walishafanya hadi wimbo ila haukutoka

“Sina tatizo na Alikiba utimu wao haunihusu, mimi mwenye nina timu True Boy,” amesema Nay wa Mitego.

“Watu hawajui tu, nilishawahi kufanya ngoma na Alikiba, kitambo sana kabla sijawa mkubwa kiasi hiki, haikutoka kabisa, nakumbuka kipindi hicho hata Alikiba hakuwa Alikiba huyu alikuwa Alikiba wa Cinderela mimi nilikuwa nimetoa wimbo unaitwa Itafahamika,” amesisitiza.

Sababu ya wengi kuamini kuwa Nay wa Mitego hana maeleweno mazuri na Alikiba ni kutokana kipindi cha nyuma alikuwa karibu sana Diamond hadi kupelekea kufanya kolabo mbili ‘Muziki Gani, Mapenzi Pesa’, hivyo wengi kuamini yeye ni timu Diamond.

Chanzo: bongo5.com