Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sina biashara na ufisadi' - nyota wa Nigeria D'banj

'Sina Biashara Na Ufisadi'   Nyota Wa Nigeria D'banj 'Sina biashara na ufisadi' - nyota wa Nigeria D'banj

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Nyota wa muziki wa Nigeria D'banj anasema "hana biashara yoyote na ulaghai" baada ya wakili wake kusema kuwa aliachiliwa kutoka kizuizini na wakala wa kupambana na ufisadi wa Nigeria - ICPC.

Alikamatwa mapema wiki hii kwa madai ya ulaghai baada ya mamilioni ya dola zilizokusudiwa kuwasaidia vijana wasio na ajira kuanzisha biashara kuripotiwa kutoweka.

"Nimeisaidia tume kwa yote ninayojua", D'Banj alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Nina imani katika uwezo wao wa kufichua ukweli," aliendelea.

D'banj pia aliongeza kuwa ameachiliwa kwa "kujitambua", ambayo ina maana kwamba hakulazimika kuweka dhamana kabla ya kuruhusiwa kwenda huru.

Wakati huo huo, msemaji wa ICPC ameambia BBC kwamba "uchunguzi unaendelea".

Msanii huyo - ambaye jina lake halisi ni Oladapo Daniel Oyebanjo - amedaiwa kuwa balozi wa chapa ya mpango wa biashara ya vijana. Hata hivyo, Wizara ya Masuala ya Kibinadamu ambayo inasimamia mpango wa N-Power, ilisema haina uhusiano rasmi na msanii huyo na kwamba madai yake ya kuwa balozi wa mpango huo ni ya upotoshaji.

N-Power ilizinduliwa mwaka 2016 na Rais Muhammadu Buhari.

Lakini wanufaika wengi wamelalamika kwa miezi kadhaa kwamba hawakuwa wakipokea ruzuku zao. Shirika la kupambana na rushwa la Nigeria lilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba "mabilioni ya naira" yameelekezwa kinyume cha sheria. Watu wengine kumi, pamoja na D'banj, wanachunguzwa, shirika hilo lilisema hapo awali.

Wakili wa D'banj alisema "ilikuwa ni aibu kwa nchi nzima kwamba tuhuma kubwa kama hii [ilitolewa] dhidi ya mtu wa umma bila ushahidi wowote".

Chanzo: Bbc