Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Simulizi ya Muniba Mazari; Usife Kabla ya Kifo Chako

Muniba Mazari Muniba Mazari

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari alimwabia Muniba Mazari hutoweza kutembea tena, mikono yako haitoweza tena kuchora picha na kamwe huwezi kupata mtoto kwa sababu ajali uliyoipata ilikuwa mbaya na kuharibu mwili wako.

Daktari hakusema haya kwa bahati mbaya kwa sababu ajali aliyoipata Muniba Mazari iliharibu uti wa mgongo, mapafu, mikono, miguu na ini. Hii ilikuwa taarifa yenye maumivu makubwa sana kwa Muniba Mazari kwasababu ilizima kabisa ndoto yake kubwa ya msanii wa kuchora.

Kwa Muniba Mazari kifo kilikuwa ni jambo muhimu, chumba alicholazwa giza lilitawala kwasababu maisha yalikuwa haya tena maana kwa binti mdogo ambaye Mwenyezi Mungu aliamua kumpa darasa ngumu kabisa kuhusu maisha.

Muniba Mazari alikaa kitandani miaka miwili akiwa hana tumaini kuu kila kitu kilikuwa kinyume nae kwasababu mwili wake ulikuwa umejaa vyuma na ndoto zilikiwa mbali na yeye baada ya ajali mbaya aliyoipata mwaka 2007.

Muniba Mazari akiwa kitandani siku moja mama yake alimwambia mwanangu hili nalo litapita Mwenyezi Mungu ana mpango mkubwa sana na wewe.

Muniba Mazari baada ya kuambiwa maneno hayo na Mama yake alitoa tabasamu la uongo ambalo ndani lilikuwa limebeba maumivu makubwa sana.

Lakini haya maneno baadae yalikuja kumfanya Muniba Mazari atoke pale kitandani na kuanza kupambania ndoto zake kwasababu ilikuwa ni lazima atimize mpango wa Mwenyezi Mungu na mbaya zaidi hakutaka kuona Mama na Kaka yake wanahuzika kwa ajili yake ilikuwa ni lazima atoke kitandani na mwili uliojaa vyuma akapambane.

Muniba Mazari mwaka 2020 kampuni yake ya sanaa ya Muniba Canvas ilikuwa na thamani ya utajiri wa Dola milioni Tano kutokana picha ambazo alikuwa na anachora, Daktari alimwambia hawezi kuchora tena Mwenyezi Mungu alimwambia utachora tena.

Pale Pakistan Muniba Mazari anaitwa Iron Lady kwasababu mwili wake umejaa vyuma na pia ameweza kufikia malengo yake licha ya kuwa kwenye kiti cha magurudumu(Wheelchair).

Usife kabla ya kifo chako -Muniba Mazari

Chanzo: www.tanzaniaweb.live