Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu ya Magufuli yaibua shangwe

1b19114bbb5638d3731b15e296e15c3e Simu ya Magufuli yaibua shangwe

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAMASHA la uzinduzi wa nyimbo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) lililofanyika juzi, lilimvutia Rais Dk John Magufuli na kupiga simu na kuzungumza na wasanii pamoja na Watanzania waliofika kushuhudia na waliokuwa wakishuhuhudia kupitia televisheni burudani hiyo ya bure.

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na maelfu ya watu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuwaweka pamoja wasanii zaidi ya 200 ambao waliimba nyimbo zaidi ya 500, Rais Dk Magufuli alimpigia simu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole na kuzungumza na hadhira iliyofurika na waliokuwa wakifuatilia kupitia vyombo vya habari.

Rais Dk Magufuli alisemaKwa kweli nimefurahi sana kwa wasanii, wana Dar es Salaam wote na Watanzania waliofika kushuhudia burudani, mambo yanayofanyika ni makubwa sana. Nilikuwa natamani ningekuwepo nijirushe rushe na kucheza kidogo, hongereni sana, nilikuwa nasikiliza kila nyimbo kwa kweli CCM ni baba lao.”

“Nilikuwa naangalia pale Msaga Msumu na kila mmoja kwa hiyo nawapongeza wasanii na watazamaji wote na nashukuru kwa sapoti tunayopata kutoka kwa wasanii na Watanzania na hii ndio Tanzania tunayotaka kuijenga.”

Tangu saa 7:00 mchana, Uwanja wa Uhuru ulifurika na wengine kukosa nafasi ya kuingia,huku askari wakifanya kazi ya ziada kuzuia walio nje kuingia ndani kuepuka maafa.

Wasanii walianza kutoa burudani mapema, ambapo mchana Ringo na kundi lake, Barnabas Elias, bendi ya Twanga Pepeta, Muumuni Mwinjuma, Msaga Sumu, Stara Thomas, Emanuel Mbasha, Adam Mchomvu, Hafsa Kazinja,Isabella Mpanda walipanda jukwaani.

Baadhi ya wengine waliotoa burudani usiku ni Harmonize, Ali Kiba, Zuchu, Peter Msechu, TMK Wanaume Family, Giggy Money, Masanja Mkandamizaji, 20 Percent, Mzee Yusuph, Jay Melody, Maua Sama, Lavalava, Rayvanny na wengine kibao.

Katika tamasha hilo ambalo lilifana, kuna matukio mawili yaliyotokea ambapo msanii Emmanuel Mbasha alipigwa gwara jukwaani na Adam Mchomvu baada ya kutokea kutoelewana jukwaani.

Akizungumzia tukio hilo Mbasha alisema: “Sina kitu kibaya nilichoongea mbele ya Adam Mchomvu na niliongea tu kwa kumtania na sikuwa na nia mbaya nimeshangaa tu nashuka jukwaani napigwa mtama namuachia Mungu.”

“Ulikuwa ni utani ila amenikosea, nimeumia kwenye mbavu, tuko hapa kwa ajili ya kufurahi lakini kwa kitendo alichokifanya amenikosea sana, mimi binafsi nimemsamehe ila amekosea,” alisema Mbasha.

Naye Adam alisema sababu ya kumpiga Mbasha ni kutokana na kumwita ‘Adam mabangi’ wakati tamasha lilikuwa mubashara na kila mtu anaangalia.

Naye msanii 20 Percent baada ya kutoa burudani ya nguvu alimtambulisha mke wake mbele ya mashabiki zake.

“Ni vizuri mtu kukutana na watu wake kwa hiyo nimejisikia vizuri na kumtambulisha mke wangu, ni jambo zuri kwani wengi walimuua kwenye kuigiza kwa hiyo nikaona ni jambo jema kupanda naye jukwaani,” alisema 20 Percent.

Mrembo huyo alishiriki tamthilia ya 20 akiigiza sehemu ambayo alionekana amekufa, hivyo alifanya hivyo kuonesha kuwa yupo hai.

Chanzo: habarileo.co.tz