Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba 'yamsajili' Misso Misondo' na Wazee wa Makoti

Ally Kamwe Msd Simba 'yamsajili' Misso Misondo' na Wazee wa Makoti

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuwa, keshokutwa Jumamosi, Desemba 16, 2023 itazindua kampeni maalum kwa ajili ya kuhamasisha mashabiki kujaa uwnjani na kuisapoti timu yao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba watacheza na Wydad Casablanca Desemba 19, katika Dimba la Mkapa ikiwa ni kampeni yao ya kusaka kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kukosa ushindi katika michezo mitatu ya mwanzo na kuambulia sare mbili na kipigo kimoja.

“Jumanne itakuwa ni MNYAMA TUESDAY, HALF DAY. Slogan ni HAIJAKWISHA HADI IISHE. It's not over until it's over. Tuna mpango wa kufanya hamasa kubwa ambayo haijawahi kutokea. Uzinduzi utafanyika tarehe 16 Desemba, 2023 eneo ni Mbagala Zakhem.

“Msafara utaanzia Uwanja wa Mkapa na magari kama 2,000. Katika uzinduzi kutakuwa na burudani nyingi kutoka kwa King Faida, Doto na balaa kubwa zaidi litasindikizwa na Misso Missondo. Miso Misondo tumechukua full package na wazee wa makoti kama 30," amesema Ahmed Ally.

Kwa upande wake, Misso Missondo amefunguka; “Jumamosi naomba Wanasimba mjitokeze kwa wingi mje mpate show ya Miso Misondo. Wale wazee wa kucheza hiyo siku mtawaona vizuri na Ijumaa tutaachia remix kwa ajili ya Simba. Naishukuru Simba kwa kunipa nafasi hii, nilikuwa natamani siku moja kufanya kazi na klabu hii."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live