Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Nyati wapagawisha washiriki tamasha la Jamafest

77104 WANYAMA+PIC

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ujio wa wanyama aina ya Simba na Nyati kwenye Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) linaloendelea jijini Dar es Salaam nchini Tanzania umeonekana kuwapagawisha mashabiki waliokimbilia banda la wanyama hao ili kuwaona.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne Septemba 24, 2019 katika Uwanja wa Taifa baada ya mashabiki kutangaziwa na mshahereshaji kuwasili kwa wanyama hao kwenye banda la wanyama katika maonyesho hayo.

Baada ya tangazo hilo, mashabiki wengi walielekea kwenye banda hilo ambalo limeezekwa kwa miti na mifuko ya nailoni lakini walikutana na kigingi kutoka kwa askari wa wanyamapori ambaye aliwataka kuwa na subira kwani wanyama hao bado hawajafungiwa kwenye mabanda yao.

Askari huyo ambaye hakutaka kutaja jina alisema wanaandaa utaratibu mzuri ili kila mshiriki apate fursa ya kuwaona moja kwa moja wanyama hao na kwa usalama.

"Tunaomba mtoke nje ili tuwashushe wanyama hawa kwanza, ambaye anajiamini kuwa na kasi ya miguu asogee karibu," alisema askari huyo kwa utani na kusababisha watazamaji hao kutoka nduki.

Hata hivyo mchakato wa kuwaona unaendelea, wanyama wengine waliopo kwenye banda hilo ni Ngamia na Farasi.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz