Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi mwili wa Director Nisher ukiwekwa kwenye nyumba yake ya milele

Nisherrr A0015 Simanzi mwili wa Director Nisher ukiwekwa kwenye nyumba yake ya milele

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako, Geor Davie akiongozana na mkewe kuaga kuaga mwili wa mtoto wao ambaye alikuwa mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya, Nic Davie katika ibada iliyofanyika kanisani hapo leo Jumamosi Desemba 16, 2023.

Nic maarufu kama Nisher alifariki dunia Jumanne Desemba 12, 2023, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali binafsi ambayo hata hivyo, haikuwekwa wazi.

Mwili wa Director Nisher umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Kisongo Arusha. Mazishi hayo yameongozwa na familia yake Nabii Mkuu GeorDavie baba yake, ndugu jamaa na marafiki.

Baadhi ya Wasanii waliofika kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele ni Ben Pol, Joh Makini, Fid Q, Dogo Janja, Gelly Wa Rhymes, Harmorapa, Gentriez na Rasi Omega.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live