Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silaha ya mauaji ya AKA yapatikana Afrika Kusini

AKA Silaha Silaha ya mauaji ya AKA yapatikana Afrika Kusini

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Afrika Kusini wamethibitisha kupatikana kwa silaha ya moto iliyotumika kumuua Msanii maarufu Kiernan Forbes, almaarufu kama AKA.

AKA aliuawa mwezi Februari pamoja na rafiki yake wa karibu, aliyekuwa mpishi na mfanyabiashara maarufu Tebello Motsoane almaarufu kama Tibz nje ya mgahawa mmoja jijini Durban.

Mkuu wa Polisi wa Kwa-Zulu Natal amekataa kutoa taarifa zaidi kuhusu ni wapi au lini silaha hiyo ilipatikana kwani itaharibu uchunguzi ambao umefikia hatua nyeti.

Mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyeshtakiwa kwa mauaji ya wawili hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live