Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikupokei gym kwangu mpaka nimjue mumeo au boyfriend wako - Denzel

Denzel Tr Sikupokei gym kwangu mpaka nimjue mumeo au boyfriend wako - Denzel

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkufunzi maarufu wa masuala ya viungo vya mwili, Denzel Trainer amesema kuwa hapokei wanawake au wadada kwenye gym yake kwa ajili ya kujifunza kabla ya kukutana na waume zao au wapenzi zao na kuzungumza nao kuhusu mipaka yake ya kazi.

Denzel ambaye ni mwalimu rasmi wa baadhi ya mastaa wakiwemo Rais Msataafu Jakaya Kikwete, Alikiba, Kajala Masanja na wengine wengi, amedai kuwa lengo la kufanya hivyo ni kulinda heshima yake kwenye kazi yake hiyo.

“Sijawahi kukutana na changamoto ya kuuza namba za watu, mtu hawezi kunivaa na kuniambia anaomba namba za mtu, sijui hata akija naweza kumjibu akajuta kwenye maisha yake. Mimi wateja wangu hawanizoei hovyo, hata watu wa nje mimi sio mwepesi sana kuzoeleka kutokana na mipaka ambayo nimejiwekea.

“Hata nikiwa gym ninafundisha client wangu, ninahakikisha kwamba kama wewe ni mwanamke umeshaondoka na mimi ndiyo nafuata. Mimi kabla sijakupokea wewe mwanafunzi wa kike, cha kwanza lazima niwasiliane na mahusiano yako kama ni mume au boyfriend wako, lazima unikutaishe naye, la sivyo sikupokei.

“Ukinikutanisha naye face to face, nizungumze naye aridhie kama ana taarifa kuwa unakuja kufundishwa kwangu na kama ameridhia. Ninalinda ile heshima ya mimi na yule aliyekukabidhi kwangu,” amesema Denzel Trainer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live