Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikumlazimisha Barnaba kubadili dini - mke

Sikumlazimisha Barnaba Kubadili Dini   Mke.jpeg Sikumlazimisha Barnaba kubadili dini - mke

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Barnaba, Raya ameweka wazi kuwa hakumlazimisha msanii huyo kubadili dini bali yeye mwenyewe ndiye aliamua.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM leo Julai 27, 2023, Raya alisema, Barnaba alipitia kipindi kigumu ambacho yeye ndiye aliyekuwa msaada wake mkubwa kuvuka kwenye kipindi hicho.

Alisema siku aliyokuwa anakwenda kubadili dini, alimfanyia kama sapraiz, hakumjulisha kabla.

"Alikwenda tu na rafiki yangu aliporudi akaniambia nimebadili dini. Nilipokea, tukaingia kwenye ndoa na hakukuwa na pingamizi lolote kutoka kwa wazazi wake licha ya kuwa ni wakristo na Barnaba amenifuata mimi kwenye Uislamu," alisema Raya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live