Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku za mwisho za uhai wa Crisda Rodriguez

Crisda Rodriguez Crisda Rodriguez.

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kabla ya kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 40 kutokana na kuugua maradhi ya saratani ya tumbo, mbunifu na mwandishi maarufu Duniani mrembo Crisda Rodriguez aliandika maneno haya akiwa kitandani na kuyahifadhi kwenye diary yake ndogo.

1. Nilikuwa na gari la gharama kubwa zaidi duniani katika karakana yangu lakini sasa inabidi nitumie kiti cha magurudumu.

2. Nyumba yangu inauza kila aina ya nguo zenye chapa, viatu, na vitu vya thamani, lakini sasa mwili wangu umefungwa kwa kitambaa kidogo nilichopewa na hospitali.

3. Nina pesa nyingi Bank lakini sasa sinufaiki na kiasi hiki 4. Nyumba yangu ilikuwa kama ngome, lakini sasa ninalala katika vitanda viwili hospitali.

5. Kutoka hoteli ya nyota tano hadi hoteli ya Almasi, lakini sasa hivi natumia muda katika Hosptali kuhama kutoka maabara moja hadi nyingine.

6. Nimetoa saini za mamia ya watu lakini safari hii kumbukumbu za matibabu ni sahihi yangu.

7. Nimekuwa na vinyozi saba wa kurembesha nywele zangu, lakini sasa sina hata unywele mmoja kichwani mwangu.

8. Kwenye ndege ya kibinafsi, naweza kuruka popote, lakini sasa nahitaji wasaidizi wawili ili kutembea hadi kwenye lango la hospitali.

9. Ingawa kuna vyakula vingi, sasa mlo wangu ni vidoge viwili kwa siku na matone machache ya maji ya chumvi usiku.

10. Hii nyumba, gari hii, ndege hii, samani hii, bank hii, sifa na umaarufu kupita kiasi hakuna hata kimoja chenye manufaa kwangu, kati ya haya hakuna kitakachonipumnzisha, "hakuna kitu halisi isipokuwa KIFO". Mwisho wa siku utajiri mkubwa kwenye maisha ya mwanadamu ni afya njema yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live