Billy Garland ambaye ni baba mzazi wa marehemu Tupac Shakur amefunguka baada ya miaka 28 tangu utoke wimbo wa maarufu wa “Dear Mama” mwaka 1995.
Jana Jumanne, The Art of Dialogue waliachia segment ya mwisho ya mahojiano na Baba huyo mzazi wa Tupac ambapo alizungumzia kitendo cha mwanaye kumuita ‘Mwoga’ kwenye mistari ya wimbo huo ulioiteka dunia.
“Mara ya kwanza nilikasirika, kwa sababu najaribu kuonana na wewe, halafu… iliniumiza sana. Kwanza, sikuwa nimekufa, hivyo kiukweli hunifahamu. Kwa sababu kama ungekuwa unanijua, basi ungefahamu kuwa sikuwa nimekufa. Hivyo nilijua kuna mtu mmoja amekudanganya.” alizungumza na kuendelea
“Baadaye, nilipokuja kufahamu kuwa kuna mtu amemdanganya, ule wimbo ulianza kuingia akilini mwangu sasa. Niliuelewa vizuri, nikiusikia sasa hivi, nacheka tu. Bado naipenda sana ile ngoma, nasikiliza nyimbo zake kila siku. Kwa wakati ule ‘Dear Mama’ iliniumiza sana, ni mwanangu.” alieleza Billy.
Billy Garland alishindwa kuonana na Tupac wala kuwa na uhusiano kama Baba na mtoto tangu Tupac ana umri wa miaka 3 hadi alipofikisha miaka 18. Hadi rapa huyo anafariki dunia 1996, bado hakukuwa na ukaribu kati yao. Kwenye mashairi yake, Tupac aliimba "No love for my daddy because the coward wasn't there/He passed away and I didn't cry, 'cause my anger wouldn't let me feel for a stranger/They say I'm wrong and I'm heartless, but all along I was looking for my father, he was gone."