Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sijawahi pata hata dola moja kutoka kwa Single Again - Harmonize

Harmonize Tz 1690451880406.jpeg Sijawahi pata hata dola moja kutoka kwa Single Again - Harmonize

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Harmonize kwa mara nyingine amerejea mitandaoni akililia utapeli unaoendelea katika majukwaa ya kidijitali ya kupakua miziki.

Msanii huyo bado anadai kwamba hajapata suluhu kuhusu kutopata maokoto kutokana na kazi zake kwenye majukwaa mbali mbali ya kidijitali ya kusambaza miziki yake.

Kupitia Instastory yake, Harmonize alitangaza kuachia ngoma tatu kwa mpigo mapema Jumanne lakini akawataarifu mashabiki wake kwamba ngoma hizo hazingeweka kupatikana katika baadhi ya majukwaa ya kusambaza kazi za wasanii kwa mifumo ya kijiditali.

Msanii huyo aliwashangaza wengi kwa kudai kwamba licha ya ngoma yake ya Single Again kuwa hit kubwa sit u barani Afrika bali hata nje, lakini bado hajawahi pokea hata dola moja kutokana na mauzo yake kwenye majukwaa mbalimbali.

“…Sijapatiwa ripoti ya mauzo yangu tangu Januari mwaka huu, sio mimi, ni Konde Gang yote. Kwa hiyo sijaona sababu yoyote ya kuwapa nyimbo zangu zingine…unaweza amini kwamba sijawahi pokea hata dola moja kutoka kwa hit kubwa ya Single Again licha ya ukubwa wake dunaini?” Harmonize aliwashangaza mashabiki wake.

Hata hivyo, mkali huyo wa Kwangwaru alisema kuwa mamlaka husika za Sanaa nchini Tanzania zinashughulikia suala hilo na hivi karibuni mambo yatanyooshwa ili wasanii wapate kufaidika kutokana na jasho lao.

Katika ujumbe wa mwisho, Harmonize alisema kwamba kwa sasa hizo ngoma mpya zitakuwa kwenye jukwaa la YouTube pekee, ikionesha kwamba pengine majukwaa mengine ya kidijitali huenda ana matatizo nayo.

Chanzo: Radio Jambo