Menu ›
Burudani
Fri, 26 Jan 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwanamuziki Shetta amefunguka kuwa licha ya kuachana na mama watoto wake lakini hajasahi kumzungumzia vibaya mama mtoto wake huyo kwa watoto.
Akizungumza na Clouds FM, Shetta amesema kuwa;
“Inapotokea wakati mwingine umebaki na watoto maswali ya hapa na pale. Kuna wakati tunakwenda site utakuta mtoto wangu wa pili anasema na anachagua chumba nikae na mama yake, chumba chake na chumba cha dada yake. Namwambia sawa.
“Simuonyeshi kama sipo na mahusiano na mama yake. Nasubiri akikua mkubwa ndio nizungumze naye. Nikikaa nao sijawahi kuwaambia mama yao ni mtu mbaya au kumponda mama yao.”
Chanzo: www.tanzaniaweb.live