Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sijamroga Barnaba, ni mahaba tu - Raya

Barnaba  Mke Raya Sijamroga Barnaba, ni mahaba tu - Raya

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya minong'ono kutawala kwenye vinywa vya walimwengu kwamba Raya amemfanyia michezo ya ndumba msanii Barbara ili amuoe, siku ya jana Raya amefunguka haya.

Amesema kwamba hajawahi kumroga Barnaba wala kumuhusisha na mambo yoyote ya nguvu za giza ili ampende zaidi, uchawi pekee alioutumia kumteka Barnaba ni kumpa mapenzi moto moto ya kitanga ambayo siyo rahisi kuchomoka, amesema kwanza anamlisha, anamuogesha na anampa mapenzi yote kiasi kwamba inamuwia vugumu kwenda kuchepuka nje.

Raya amewashauri wanawake waachane na mambo ya uchawi badala yake wapambane na kuwahudumia wapenzi wao ipasavyo ili wasiachwe na wasichepuke.

Amesema amepanga kumzalia Barnaba watoto watatu tu kwa kuwa tayari Barnaba ana watoto wengine wawili akimuongezea wa kwake watatu watakuwa wanamtosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live