Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Siijui bedroom ya Harmonize, bifu la Alikiba" 20%

20 "Siijui bedroom ya Harmonize, bifu la Alikiba" 20%

Wed, 3 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa BongoFleva 20 Percent amepiga stori na eNewz ya East Africa TV na kufunguka mambo makubwa matatu ikiwemo muziki, uwezo wa msanii Harmonize na bifu la Producer Man Water na msanii Alikiba.

Kuhusu msanii Harmonize, 20 Percent amesema anaamini muziki kutoka kwa Konde Boy na huwa hangalii kipaji kwa sababu hajui kipaji chake anakipelekaje.

"Siijui bedroom ya Harmonize ila ameachia video ya wimbo wa "fall in love" naisikiliza sana, ile ndiyo ngoma ya mapenzi kwa sasa, Konde ni mwanamuziki na naamini kwenye muziki wake kuliko kipaji chake kwa sababu sijui kipaji chake anakipelekaje na hatuandiki vitu vinavyofanana" amesema 20 Percent

Aidha 20 Percent amezungumzia tofauti iliyokuwepo kati ya Producer Man Water na Alikiba kwa kusema "Sipendi kuongelea bifu zisizonihusu au vitu vya watu ila nina uhakika Man Water yupo sahihi kuliko Alikiba, kwa sababu mwenye jukumu la kutoa ngoma ni mwanamuziki japokuwa producer ana haki zake za msingi, nyimbo ambazo Alikiba amewahi kuzifanya kwa Man Water ndiyo nyimbo zake bora kuliko zote alizowahi kuzifanya"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live