Aliyekuwa mke wa mpigapicha Lukamba, Shuu, amemvaa aliyekuwa mke mwenziye kwa kusema, hajambadilisha Lukamba sababu alimkuta akiwa tayari na maisha yake.
Shuu alisema, amemsikia akisema maneno hayo kwenye media kwamba kambadilisha Lukamba wakati yeye na Lukamba ndio wametoka mbali.
"Lukamba mimi tumekutana akiwa bado hana hata umaarufu, hajawa mpigapicha. Tulikuwa kwenye uigizaji, tukaanza maisha pamoja hadi baadaye tukaoana. Hajamtengeneza Lukamba kwa chochote, sema yeye ndiye katengenezwa na Lukamba," alisema Shuu.
Cessy alihojiwa hivi karibuni akadai kwamba yeye hakuwa mwanamke wa kuletewa nyumbani kama Shuu na kwamba yeye ndio kambadilisha.