Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shusho: Kuwa karibu na Harmonize sio tatizo kwangu

HARMONIZE NA SHUSHO Shusho na Harmonize

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Injili Tanzania, Christina Shusho amesema kuwa kwa miaka mingi amekuwa karibu na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz na Harmonize, hivyo haoni kama kuna tatizo kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema.

"Mimi sijali watu watasema nini kikubwa najua ninachofanya siyo dhambi, kwa nyakati tofauti nimekaa na Diamond Platnumz na nimekaa na Harmonize, hawa ni watu poa sana tofauti na watu wanavyowachukulia mitandaoni.

"Nimekaa na Harmonize sana hasa kipindi cha mgogoro wake na Kajala nilimshauri vitu vingi sana lakini hata siku moja hajawahi kumzungumzia vibaya Diamond, zaidi anamsifia na anamshukuru kwa kumfikisha alipo leo.

"Mimi kumuita Nabii Mkuu Geordavie "Mfalme" siyo shida, na wanaojaji lile tukio wana elimu ndogo ya dini, wana msongo wa mawazo hawajui wanachokizungumza wanaona wakinisema ndio mioyo yao inapona, Geordavie ni baba yangu wa kiroho tumetoka mbali sana, amenilea sana siwezi kuacha kuwa karibu nae.

"Nimezunguka dunia nzima nimebakisha mabara mawili tu ila sipendi kujionyesha kwa sababu mimi siyo mtu wa kujigamba, lakini nina watu karibia dunia nzima.

"Nimetoa Album yangu mpya inaitwa (Hararat) ina nyimbo 24 na inapatikana YouTube naomba mkasikilize nyimbo hizo," amesema Christina Shusho, Msanii wa muziki wa Injili Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live