Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shoo yamfanya Usher Raymond aache pombe

Usher RAymond.jpeg Shoo yamfanya Usher Raymond aache pombe

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Usher Raymond ameamua kuacha matumizi ya Pombe na vinywaji vyenye sukari kwa ajili ya kujiandaa na onesho la ‘Super Bowl Halftime’ litalofanyika Allegiant nchini humo mwezi Febuari 11 mwaka huu.

Inaelezwa kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 45 ameamua kuacha vitu hivyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki katika onesho hilo alilokuwa akilisubiri kwa zaidi ya miaka kumi.

Mwanamuziki huyo amewahi kufanya nyimbo kama OMG, Good Good, ‘Hey Daddy’, ‘My Boo’, ‘Dientes’, ‘Yeah!’, ‘U got it Bad’, na nyingine nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live