Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shoo ya Werrason yazua sintofahamu

9838 Werason+pic TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unakumbuka ile shoo ya Werrason iliyoahirishwa mara mbili na kushindwa kufanyika kutokana na mvua za masika zilizonyesha jijini Dar es Salaam kwa takriban siku nne mfululizo? Sasa mkali huyo wa masauti anatua tena kutikisa Jukwaa la Life Park Mwenge kwa mara nyingine, lakini kama una tiketi ulinunua wakati ule fahamu kuwa hazitambuliki tena.

Mwandaaji wa shoo hiyo, Yale Ngos anasema hazitambui tiketi hizo na kwamba mashabiki wanaotaka kumuona Werrason wakate upya.

Mkurugenzi wa Basata, Godfrey Mngereza amesema hawajapata malalamiko kutoka kwa mashabiki na iwapo watapata taarifa hiyo rasmi watachukua hatua.

“Hatujapata taarifa hiyo sisi bado tunayatambua makubaliano ya awali kwamba mashabiki watunze tiketi sasa hili halijatufikia,” anasema Mngereza.

Chanzo: mwananchi.co.tz