Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shoo ya King Kiba Tigo- Fiesta yamliza shabiki

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa kizazi kipya, Ali Kiba au King Kiba amemtoa machozi shabiki wake msichana kuanzia mwanzo hadi mwisho baada ya kupanda jukwaani.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:00 alfajiri ya kuamkia leo Jumapili Desemba 23, 2018 msanii huyo alipoitwa kuimba jukwaani wakati wa kilele cha tamasha la Tigo-Fiesta lililofanyika Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Mara ya kwanza alianza kama utani dada huyo aliyejulikana kwa jina moja la Ene, kuonyesha hisia baada ya Kiba kupanda na wimbo wa ‘Seduce’ na baadaye alipoendelea kushusha vibao vingine mfululizo mwanamke huyo wa umri kati ya miaka 27-32 alichomoka alipokuwa amekaa na kuvamia jukwaa.

Askari waliokuwa wanaimarisha ulinzi eneo hilo walimkamata ili kumrudisha, lakini Kiba alipomuona aliwaambia wamwachie ndipo aliposalimiana naye huku akiwa anabubujikwa machozi jukwaani hapo kwa dakika kama tatu kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Hata hivyo, Mwananchi  lilizungumza na dada huyo kisa cha kuangua kilio amedai anampenda sana Kiba na kumuona uso kwa uso kisha kuweza kushikana naye mkono ni tukio ambalo bado haliamini.

“Yaani ninavyokuambia huyu msanii ninampenda sana hata sijui nielezeje, natamani hata niwe naishi naye na kuwa naye kila mahali ninapokwenda,” amesema dada huyo huku akiendelea kumwangalia Kiba na kububujikwa machozi.

Katika tamasha hilo, Ali Kiba aliimba akiwa amembatana na wasanii kutoka lebo ya Kings music kwa dakika 45 mfululizo bila kupumzika.

Mwisho.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz