Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sholo Mwamba: Man Fongo ndiye mshindani wangu

Fongooo 136 Sholo Mwamba na Man Fongo

Sat, 29 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa singeli nchini Sholo Mwamba amesema anatamani msanii mwenzake Man Fongo arudi katika ubora wake katika muziki wa singeli ili kuwe na ushindani kama walivyokuwa zamani.

Sholo amesema kwa sasa yeye ndiye msanii pekee anayefanya vizuri katika muziki huo na haoni ushindani wowote kama ilivyokuwa kipindi Man Fongo alipotoa wimbo wa ‘Hainaga Ushemeji’ naye akatoka na wimbo wa ‘Ghetto’.

“Man Fongo ndiye alinipa ushindani mkubwa sana katika singeli maana kipindi kile ametoa wimbo wa ‘Hainaga Ushemeji’ kila mtu alikuwa anauimba mimi nikafikiria namna ya kuja zaidi yake nikatoka na ‘Ghetto’ onyesha funguo ngoma hizo mbili zikawa juu zikashindana sana na zilikuza muziki wa singeli lakini kwa sasa hakuna ushindani kama ule;

“Mimi kwa sasa nimewekeza mno katika muziki wangu maana ndiyo maisha yangu natoa kazi nzuri na video zenye viwango ndiyo maana kwa sasa nikitaka kumshirikisha msanii yeyote kutoka bongo fleva hatokataa kwa sababu ya uwezo wangu katika singeli”

Wito wangu kwa wasanii waliopo katika muziki wa singeli waache mazoea muziki umebadilika unataka uwekezaji hivyo chochote wanachopata kupitia kazi za muziki huo wawekeze kwenye utunzi wa nyimbo kali na pia video zao ziwe na ubora waache usela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live