SHINDANO la Mwanamitindo bora 2021/2021 'Tanzania Top Model' limezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam
Mwandaji wa shindano hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya mavazi ya 'Paka Wear Fashion', Gymkhana Majaliwa, amesema shindano hilo litarushwa katika kipindi cha Luninga (Reality Television Show) kwa muda wa miezi mitatu.
Alisema lengo la kurushwa kwa miezi mitatu ni kutoa nafasi kwa wananchi na wadau wa mitndo kufuatilia kipindi na kuweza kupata uhuru wa kupiga kura ya kumuongezea mshiriki nafasi ya kuibuka mshindi.
Alisema, kura zitapingwa kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi au kwenye mitandao.
"Shindano la kumtafuta Mwanamitindo bora wa fano wa Tanzania ssimu huu 2021/2022 litawashirikisha Wabunifu Chipukizi wa Mitindo ya mavazi kuanzia ngazi ya robo fainali kwa kuwa na nafasi 3)." alisema na kuongeza
"Lengo ni kukuza vipaji, kuongeza kipato, kurudusha uchumi wa mtanzania kwa mtanzania mwenyewe,kulinda utu wa mwanamke wa Kitanzania na kuonesha ubunifu kitaifa na kimataiafa.
Kwa upande wa Meneja miradi wa kampuni ya Paka Wear, Adili Kigoda, alisema shindano hilo litaendeshwa katika kanda teule mbalimbali ikiwemo Tanzania Bara na Zanzibar.
"kauli mbiu yetu ni 'Uanamitindo wenye malengo" hivyo mshindi ataingia mkataba na Kampuni yetu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kwa lengo la kufanya kazi za sanaa ya mavazi na kijamii.
Aidha, zawadi kwa washindi ni pamoja na mshindi wa kwanza kupata pesa taslimu sh milioni 5, mshindi wa pili na wa tatu kila mmoja atazawadiwa sh milioni 2 na mshindi wa wanne hadi wa 10 watazawadiwa cheti cha ushiriki.
Naye Afisa sanaa kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Selemani Mabisso, alisema kama serikali watahakikisha wanasimamia maadili na kuendeleza utamaduni wa mtanzania kwa nyanja mbalimbali ikiwemo mitindo na ubunifu.