Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole awalipua wasanii wanaolalamikia tuzo

SHILOLE Bnm Shilole awalipua wasanii wanaolalamikia tuzo

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shilole awajia juu wasanii wanaolalamikia tuzo “Fanyeni kazi acheni udananda”

Msanii wa muziki na mjasiriamali Zuwena Mohamed 'Shilole' amepongeza waandaji wa tuzo kwa mchakato mzuri huku akiwataka wanaolalamika kufanya kazi.

Muimbaji huyo ambaye ametajwa kwenye kipengele cha msanii bora wa kike BongoFleva, amedai wasanii wanalalamika kwa kuwa hawajatajwa.

“Na mkileta mzaha na tuzo nachukua!,” alisema Shilole.

Aliongeza “Wote mnaopiga kelele ni kwa sababu hampo kwenye kipengele chochote. @basata.tanzania msiyumbishwe fanyeni kazi yenu! Mnataka kujizima data wakati sitaki mazoea ilikuwa hit song mwaka jana. Watoto wa kiume fanyeni kazi, udananda utawaponza. ndio Shishi Master kabisa napiga miguu yote.. ndegelec in @hajismanara ‘z voice,”

Kuhusu malalamiko hayo, Basata walitoa taarifa ya kwamba mchakato wa kuwapata wasanii katika uteuzi wa tuzo hizo ni kwa njia ya wasanii kujipendeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live