Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole akataliwa kuwa Jaji wa Bongo Star Search

SHILOLE Bnm Shilole akataliwa kuwa Jaji wa Bongo Star Search

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maneno ya mdau wa masuala ya muziki na burudani; Nimeona leo Madam Ritha kutoka Bongo Star Search amezindua Rasmi Msimu wa 13 wa Shindano hilo.

Kiukweli nimeshangaa sana hasa list ya Majaji ambayo imetambulishwa leo hii, yupo Rayvanny, Nandy, Jux, Fid Q, Shilole na Barnaba.

Katika hii list wanaojua muziki Nje na Ndani ni wachache sana, Hapo nampitisha Fid Q na Barnaba lakini wengine waliobakia wamekaa kimchongo tu, hivi shilole na muziki wapi na wapi?

Mtu mwenyewe kila ngoma anaandikiwa, Kuimba hovyo halafu leo hii anapewa jukumu la kujaji vijana wanaoimba! huu ni upotezaji wa hela, ni bora wangemfata hata mwanafunzi mwaka wa kwanza pale TASUBA kuliko kumweka Shilole.

Kujua kuimba sio kujua kujaji mtu, hapo ndipo tunapopotea, Jaji lazima ajue vitu vingi, upigaji sahihi wa Vyombo vya muziki, Key, notes, pitch, tone, rhythm, N.k sasa shilole na baadhi yao hapo wanajua hivi vitu?

By Hopetyga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live