Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole: Nilitoa hati ya nyumba nipate ada ya mtoto

Shiloleeee S Shilole.

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na Mjasiriamali Shilole amesimulia alivyowahi kuweka hati ya nyumbani rehani ili apate pesa ya kulipia Watoto wake ada ya Shule kwani iliwahi kufika mahali alikuwa anapambana na bado anajikuta anakosa hela ya ada mpaka kutumia njia nyingine za kiupambanaji.

Shishi amefunguka hayo kwenye mahojiano maalum jana katika ofisi zake za Shishi Food ikiwa ni saa machache baada ya kutangaza furaha aliyonayo baada ya Mtoto wake Joyce kufaulu kwa kupada division 1 ya 7 katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo.

Katika hatua nyingine Shilole ametangaza ujio wa Festival yake ya vyakula vya asili itakayokuja hivi karibuni baada ya kuanzisha mtindo wa kupika vyakula vya kiasili vya kila Kabila kila Alhamisi ambapo alianza na Wachaga na Wiki hii amepika vya Wahaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live