Msanii maarufu wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema kuwa katika biashara yake ya chakula alianza kwa kuuza sahani chache lakini leo hii anapata pesa nyingi na amekuwa maarufu hasa kwenye shughuli kubwa.
“Nilianza kwa sahani chache nilizouzia rafiki zangu, nikasogea kuwa na sehemu ndogo, tukawa na eneo letu pale Morocco. Baadae nilifyeka eneo lililokuwa pori pale Kinondoni, na kuweka kujenga Shishi Food ya sasa (Dar es Salaam).
“Kwa majaaliwa ya Mungu na support yenu ndugu zangu, nimeweza kubadilisha eneo lingine hapa Dodoma, tumejenga kuanzia mwanzo na kupata kitu kizuri. Video hiyo inaonesha eneo lilivyokuwa.
“Nawashukuru sana lakini bado nawaomba support yenu, msiniache mimi mtoto, dada, mdogo na rafiki yenu: hebu Jumapili jioni njooni tuzindue pamoja eneo jipya hapa karibu na shopaz Dodoma na tulipe nguvu sana. This is before tusubiri after," amesema Shilole.