Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole: Nilianza mapambano nikiwa mdogo

Ab15cff2fb38eca8a42edd39b39930cc Shilole: Nilianza mapambano nikiwa mdogo

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema maisha magumu aliyokulia yalimfanya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi akiwa bado mdogo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Shilole alisema maisha aliyopitia hataki yawakute watoto wake ndio maana amekuwa akiendelea kuwapigania wasome wafikie ndoto zao.

Alisema mtoto wake wa kwanza alimpata akiwa na umri wa miaka 14 na wa pili miaka 19 na amekuwa akipambana yeye mwenye kama baba na mama kuwalea.

“Niliishi peke yangu na watoto kwa muda mrefu, nawalea mwenyewe na nimeshazoea mapambano kupigania maisha ya watoto wangu kusudi watimize ndoto zao,”alisema.

Alisema anashukuru kuona watoto wake hawamwangushi wamekuwa wakifanya vizuri darasani.

Shilole mara nyingi amekuwa akihadithia maisha aliyopitia ili iwe funzo kwa wanawake wengine wanaokutana na changamoto kutokata tamaa bali kupambana.

Nyota huyo amekuwa akijishughulisha na biashara ya mama ntilie na wala hajawahi kuona aibu kuelezea kile anachokifanya bali amekuwa akiitangaza biashara yake watu wamuunge mkono, kwani mbali na muziki humsaidia kuendesha maisha yake na watoto wake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz