Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole: Kipigo cha Uchebe kilizidi

C121a65e6e0334ec82ab2ee97a40913b Shilole: Kipigo cha Uchebe kilizidi

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu Shilole, amesema kurudiana na mume wake Uchebe ni kama kuendesha gari ambalo lipo kwenye ‘handbrake’.

Shilole aliyasema hayo juzi baada ya kutangazwa kuwa Balozi wa bidhaa ya nazi inayoitwa GSM Coconut Cream, ambapo alisema ni nazi nzuri ambayo inaweza kumrudisha mliyeachana ndipo akaulizwa iwapo na yeye hiyo nazi inaweza kurudisha mapenzi kwa Uchebe.

“Kule nilishatoka na kurudi ni sawa na kuendesha gari ambalo lipo kwenye ‘handbrake,” alisema.

Pia Shilole alisema sababu iliyomfanya kupigwa na Uchebe na kupata majeraha ni baada ya kumuuliza kuhusu taarifa za yeye kuzaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

“Mimi nikiwa Sabasaba nahangaika kwa ajili ya familia yangu na yeye nilimpigia simu nikamuuliza mume wangu kuna habari nimezisikia kuna dada umezaa naye yuko Africana sijui Africa Sana, akanijibu ndio si hutaki kuzaa na mimi? Niliingia kwenye gari nikalia sana.”

“Nikamaliza biashara yangu nikarudi nyumbani, nikaingia ndani nikamkuta anacheza playstation, nikamwambia Asalaam Aleykum mume wangu hakuitikia akaendelea kucheza, nimelala zangu niliamshwa na ngumi ya sikio, sijakaa sawa nikapigwa ngumi nyingine.”

“Kupigwa na wanaume sijaanza leo, tangu mwanaume wa kwanza aliyenioa nikiwa na umri wa miaka 18 alikuwa ananinyanyasa na kunipiga sana, ila kipindi hiki cha Uchebe imezidi,” alisema Shilole.

Chanzo: habarileo.co.tz