Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilole: Hatujarudiana, nitaelezea yote

Shilole+pic Shilole na Uchebe

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahBaada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Shilole kurudiana na mumewe mwenyewe afunguka.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa Desemba 2017 na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.

Shilole ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohammed, hivi karibuni aliibua gumzo baada ya kuanika vitendo vya unanyasaji wa kipigo ambayo amekuwa akifanyiwa na mume wake wa ndoa Ashraff Uchebe na kutangaza rasmi asijulikane kama mume wake.

Kitendo hicho kilisababisha watu mbalimbali kupaza sauti zao kukemea jambo hilo wakiwemo wasanii,watu maarufu na wanaharakati wa haki za binadamu na wanawake.

Hata hivyo wakati ukimya ukiwa umetawala wa hatua gani Shilole kachukua zaidi baada ya sakata hilo, kuna Video imekuwa ikisambaa kwa kasi leo Jumanne Julai,14 2020 katika mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa na mmiliki wa saluni inayohudumia wanawake ambaye ni maarafufu kwenye mitandao ya kijamii akiwaonyesha wakiwa kimahaba na mume wake huyo huku akisema amerudi na amemsamehe.

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz