Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shetta endelea na siasa tu - Lukamba

Shettah Sd Lukamba Shetta endelea na siasa tu - Lukamba

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya staa wa Bongo Fleva, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta kuwataka wasanii wa Bongo kuacha kushobokea mziki wa Amapiano wa Afrika Kusini huku akisema kuwa ni wakati umefika wa kuiangamiza rasmi Amapiano.

Shetta alienda mbali zaidi na kudai kuwa huko Afrika Kusini hakuna ngoma za Amapiano za Watanzania zinazopigwa kwenye radio wala clubs zao, msanii mwenzake Lukamba amemjibu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"Tunachanganya wivu na mziki kwani South (Afrika Kusini) wao wamekuwa wakina nani wasipo piga, ni wao tutafanya mpaka wajute. Hata mlivyo kuwa mnafanya bongo fleva kelele za kutopigwa kwa nyimbo zilikuwepo tu.

"Ili piano zife anzeni na ma-dj wote na ma-producer wote iwekwe mikakati kama waliyo iweka South, kwa mujibu wako kweli zitakufa.

"Wanaopenda piano ni wengi sana achana na watu wachache wanao taka kubishana na soko la mziki. Mimi nafikiri bro ungeendelea na siasa tu kaka angu," amesema Lukamba.

Una maoni gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live