Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shetta aweka wazi kubwagana na mkewe, ashauri wasanii wanapoachana wasikimbile Instagram

Shetta Pic Data Shetta aweka wazi kubwagana na mkewe

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii Nurdin Bilal maarufu Shetta, ameshauri wasanii kutopenda kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram pale wanapoachana kwani huo nao ni ukatili wa na unyanyasaji wa kijinsia.

Shetta ameyasema hayo leo Jumatano Juni 23, 2021 wakati alipokuwa akizindua shirika lake la 'Sawa Initiative Tanzania' linalolenga kupingana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Msanii huyo aliyewahi kutesa na vibao mbalimbali ikiwemo Mdananda, Kerewa, Namjua na Shikorobo, amesema hata yeye mwaka jana aliachana na mke wake walioishi naye miaka tisa, lakini anashukuru waliweza kuliweka sawa hilo wenyewe bila kukimbilia mitandaoni.

"Ilikuwa ni hatua ngumu sana kwangu ukifikiria ni mwanamke tumeishi naye miaka tisa na tuna watoto wawili naye, lakini sikutaka haya kuyapeleka huko mitandaoni badala yake tuliyamaliza wenyewe.

"Pia nashukuru kwa sasa tumebaki kama wazazi katika kulea watoto na tumekuwa tukitoka nao out wakati mwingine lengo ni kuwafanya watoto wetu wasijisikie vibaya na waone uwepo wa wazazi wote katika kuwalea," amesema Shetta.

Akizungumzia kuhusu shirika lake, msanii huyo  amesema ni katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umezidi kushamiri katika jamii.

Katika kufanya kazi hiyo, amesema wameanzisha klabu mashuleni na njia kubwa watakayoitumia katika kueneza elimu ya kupambana na vitendo hivyo ni kutumia muziki.

Katika uzinduzi huo wasanii mbalimbali walishiriki akiwemo Barnaba, Dogo Janja, Madee, Kala Jeremiah, Mwasiti, G Nako, Ommy Dimpoz na wengine wengi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz