Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shepu matata yamponza ticha

Mwalimu Mklss Shepu matata yamponza ticha

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa sanaa huko New Jersey nchini Marekani amejikuta kwenye mzozo mkali na wazazi baada ya wazazi hao kumkataa kutokana na shepu lake matata wakidai linawachachafya wanafunzi darasani.

Mwalimu huyo maarufu kwenye mitandao ya kijamii akitumia jina la Toy Box Dollz amekosolewa vikali kwa umbo lake alivyoumbika huku wazazi wakimtuhumu kuwa msumbufu wa akili za watoto wao.

Umbo lake na mavazi yake ni sababu kubwa kuwa inawafanya mpaka watoto wabaki kumuangalia mwalimu badala ya kupata kile anachokifundisha darasani.

Wazazi hao wanasema umbo lake na muonekano wake ni tatizo kwa watoto wao. Mwalimu huyo ni maarufu mno kwenye Instagram ambapo yeye huposti mara kwa mara picha zake akiwa darasani na pia akifanya shughuli nyingine za kufurahisha akiwa nje ya shule.

Baadhi ya wazazi wanadai afukuzwe kazi huku wengine wakisema avae tu nguo zinazoficha maumbile yake.

Chini ya Sheria ya New Jersey na Sheria ya Shirikisho la Kazi, itakuwa kinyume cha sheria kwa shule kumfukuza kazi mwalimu kulingana na sura yake, ambayo labda ndiyo sababu na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya malalamiko yanayodaiwa ambayo yametolewa kuhusiana na sura ya mwanamke huyo na umbile lake.

Taarifa hiyo imechapishwa na majarida na blogu nyingi duniani huku wengi wakivutiwa na umbo la mwalimu huyo na kusema kwamba haina haja ya wazazi kukasirika kwani wanafunzi anaowahudumia bado ni wadogo kufikiria mpaka kiwango cha mapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live