Changamoto ya kukosa mtoto kwa wakati katika ndoa imetajwa kuwa moja ya kisababishi kikuu cha migogoro na mateso katika ndoa jambo linalosababisha baadhi ya ndoa kukosa amani na familia kusambaratika.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 29, 2023 na Shekh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke kwenye ibada ya Eid el Adh’haa iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
“Mwenyezi Mungu ndiye ampaye watoto binadamu. Lakini hawa wanaokosa watoto katika ndoa wanaishi kwa mateso makubwa sana kutoka kwa mashemeji, mawifi, ndugu na jamaa na hata kwa wanaume wenyewe waliowaoa kwa hiyo nawaasa katika hili wakumbuke kisa cha nabii Ibrahim na Salah walikuja kupata motto uzeeni,” amesema.