Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Sharuk Khan afunga umeme vijiji 7

Shah Rukh Khan And His Charitydonation Works 1534857279 725x725 Sharuk Khan afunga umeme vijiji 7

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JeWajua? Mwaka 2009 staa na muigizaji maarufu wa nchini India, Sharuk Khan alitoa msaada kwa kupeleka umeme wa solar kwa vijiji saba nchini humo, umeme ambao ulinufaisha familia 270 zilizoweza kuona mwanga kwa mara kwanza ikiwa ni takriban miaka 61 kupita tokea wapate uhuru.

HISTORIA FUPI

Shah Rukh Khan alipoingia jiji la Delhi kwa mara kwanza kwa ajili ya kutafuta dili za uigizaji, hakuwa na mtu yoyote wa kumtegemea na pesa pekee aliyokuwa nayo ilikuwa dollar 18 (sawa na shilingi elfu 45 za kibongo kwa hivi sasa.)

Mara nyingi alitupiwa vitu vyake nje baada ya kushindwa kulipa kodi na alikataliwa mara kwa mara na waongoza filamu kila alipokwenda kwenye usahili kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuigiza wakimuona hawezi.

Nyota yake ilianza kung'aa taratibu pale alipokuja kupata ofa za kuigiza uhusika ambao waigizaji wengi wakubwa walikataa kuigiza.

Mpaka leo hajasahau kuwashukuru wote waliomsaidia katika safari yake ya maisha na ameendelea kuwa mnyenyekevu hata baada ya kuwa staa mkubwa duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live