Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shape za michongo zatikisa Bongo

Wema Muna Shape za michongo zatikisa Bongo

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKATI msanii wa Bongo Movies, Rose Alphonce almaarufu Muna Love akimrudia Mungu wake na kumuomba toba kwa kile alichokifanya huku akienda mbali zaidi kwa kuwasihi watu wasifanye sajari, hatimaye shepu hizo bandia, zinazidi kutikisa Bongo, IJUMAA lina ripoti kamili.

Wiki kadhaa zilivuja tetesi kwamba mwanamama Aunt Ezekiel naye amekwea pipa kwenda nchini India kwa ajili ya kutengeneza shepu, lakini mwenyewe alikanusha kabla ya jana kukiri kufanya hivyo.

Kupitia Gazeti la IJUMAA tunakuletea listi ya baadhi ya mastaa Bongo wanaodaiwa kutengeneza shepu kwa sajari ama nchini Uturuki au India na wengine hapahapa Bongo na namna zinavyoonesha kushtua wengi na kushawishi wengine kufanya hivyo;

AUNT EZEKIEL

Mapema wiki hii, Aunt ameshtua wengi baada ya ile shepu yake ya mwanzo kubadilika; yaani amekuwa na shepu matata mithili ya Beyonce wa Jay Z wa Marekani. Licha ya madhara yote yanayotajwa kuweza kumpata mtu anayefanya upasuaji huo, lakini Aunt anaonekana kutokujali na ndiyo kwanza anafurahia mwonekano wake huo mpya.

MUNA LOVE

Miongoni mwa watu ambao walikuwa mstari wa mbele kujinadi kuwa amefanya upasuaji wa viungo vingi kwenye mwili wake ikiwemo dimpozi, tumbo, shepu, midomo na sehemu nyingine, ni pamoja na mwanamama Muna Love. Na kweli baada ya muda alivujisha picha na video za kabla na baada ya upasuaji huo, lakini baada ya muda aliripotiwa kuwa ni mgonjwa na kuwasihi watu wasiende kufanya sajari hizo kwa sababu siyo nzuri kiafya na anajuta kufanya hivyo.

ZARI THE BOSS LADY

Zari amejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuzaa watoto wawili na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz. Naye ni miongoni mwa mastaa ambao hivi karibuni wanadaiwa kufanya sajari ya shepu yake na hata baada ya kuandamwa mitandaoni aliibuka na kusema watu waache ushamba kwa sababu sajari siku hizi ni jambo la kawaida tu; yaani kama mtu anavyokwenda sokoni kununua maharage hivyo wasiongee na kuona kama ni kitu cha ajabu.

TANASHA DONNA

Kama ilivyo kwa Zari, mwanamama Tanasha naye amepata umaarufu mkubwa baada ya kuzaa mtoto mmoja wa kiume na Diamond aitwaye Naseeb Junior. Miaka miwili iliyopita wakati akiwa Bongo kabla ya kurejea nchini kwao, Kenya, baadhi ya watu walionekana kumsema kuhusu shepu yake kuwa siyo matata, lakini naye mwaka jana alidaiwa kwenda kufanya sajari ya kutengeneza umbo lake na sasa ana umbo namba nane na kiunio cha nyigu.

HAMISA MOBETO

Hamisa ndiye alikuwa mrembo wa kwanza Bongo kuamsha mastaa wenzake baada ya kudaiwa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kufanya upasuaji na kutengeneza shepu.

Baada ya kuposti picha na video akiwa nchini humo watu wengi walionesha kushangazwa na namna alivyoumbika ghafla, lakini huwezi amini licha ya kwamba shepu yake ya sasa inaonekana bomba zaidi kuliko ile ya mwanzo, lakini mwenyewe amekuwa akikanusha mara kwa mara kuwa umbo lake amerithi kwao na wala siyo feki kama watu wanavyosema.

POSHY QUEEN

Mwanamama Poshy Queen ndiye anatajwa kuwa tishio kutokana na umbo lake lilivyojigawa na kuwa na kiuno chembamba. Madai yaliyopo ni kwamba, kabla ya kufanya sajari umbo lake lilikuwa tofauti kabisa na alivyo sasa kwa ushahidi wa picha zake za zamani.

VERA SIDIKA

Hata hivyo, huwezi kuhitimisha listi hii bila kumtaja mwanamama maarufu Afrika Mashariki akitokea nchini Kenya, Vera Sidika kwani anatajwa kuwa ndiye ‘mwalimu’ wa wanawake wengi waliofanya sajari kwa kuwa wanamtazama alivyokuwa awali na sasa ana umbo namba nane na kuvutia wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live