Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Shangazi Kaja' ya Diamond gumzo Afrika nzima

Diamond Shangazi Diamond Platnumz

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameiteka mitandao ya kijamii Barani Afrika kutokana na vazi alilolivaa katika video ya wimbo wa #Oka aliomshirikisha Mbosso.

Diamond alivalia vazi lililotengenezwa kwa mifuko ya kubebea vitu, maarufu kwa jina la Shangazi Kaja, na kuzua gumzo mitandaoni, wengi wakivutiwa na ubunifu huo.

Inaonekana mfuko wa Shangazi kaja ni maarufu Barani Afrika huku ukiwa na majina tofauti tofauti kila eneo.

Mashabiki wa Diamond kutoka pande mbalimbali ikiwemo Tanzania yenyewe, Nigeria, Rwanda, Uganda, Congo Birundi na nchi nyingine nyingi za Afrika wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusiana na vazi hilo.

Wabunifu wa mavazi wanasema huenda Diamond alifanya makusudi kuvaa vazi hilo kwani alijua tu lazima litazua gumzo hivyo kufanya video hio ifanye vizuri zaidi.

Video hio kwa sasa inashika namba moja kwenye mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji zaidi ya milioni 2 na ikiwa ni siku ya tatu tangu iwekwe katika mtandao huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live